Search

Thursday, March 3, 2016

Sanches asema asernal hawajiamini

1 comment
          hii ni mara  baada  ya arsenal  kushindwa  kuchomoka  wakiwa  ndani  ya  uwanja  wao  wa  emirates  mbele  ya swansea  kwa  kukubali  kichapo  cha  goli  2-1 kutoka  kwa Wayne Routledge na Ashley Williams hii ni  pamoja  na  arsenal  kuwa  wa  kwanza  kupata  goli  kutoka  kwa  mchezaji  wao  Joel Campbell katika dakika ya 15  mchezo.
  hivyo  mchezaji huyo  wa  arsenal Alexis  sanchez  alisema  "nadhani  tunaweza kushinda kombe  hili  la ligi na  wachezaji  tulionao  lakini  kuna  aina  fulani  ya  njaa tunaikosa  tunapokua  uwanjani, tunatakiwa  kuingia  uwanjani  tukiwa  kama  watu  ambao  tumeshafungwa  goli  moja  mbele  ili tupate  ari na  kasi ya kutafuta  ushindi"
"naukumbuka  ssana  mchezo  kati yetu  na  manchester united mwaka jana  tuliingia  tukiwa  na  njaa ya  magoli  kitu  ambacho kilifanya  timu  kucheza  kwa  nguvu zote  na  kasi  ya  kushambulia  kiasi kwamba  ndani  ya  dakika  ishirini tu  tulikua  tumeshapata  magoli matatu mbele"aliongeza  alexis sanches,
hivyo  sanches alimaliza  kwa  kusema  kuwa  anadhani  waoo kama arsenal  wanakosa  kujiamini  kama  wanaweza  kuwa  mabingwa  wa  ligi  hiyo  kwa  msimu  huu wa 2015/1016.
kwasasa  ligi  kuuu uingerza  inaongozwa   na  leicister city  kwa  point 57 ambaye  pia alishindwa  kupata  ushindi akiwa  nyumbani   na  kuambulia suluhu ya 2-2 dhidi  ya  west brom, ikifuatiwa  na  Tottenham kwa  pointi 54 mara  baada  ya  kukubali  kichapo  cha  goli  1-0 kutoka  kwa  west ham.....

1 comment :

hot weekly news

toniking wed designer

toniking wed designer