Search

Monday, March 28, 2016

Wenye tumbili wao walia na serikali..

No comments


Wenye tumbili wao walia na serikali



CHAMA cha Wasafirishaji wa Nyara Tanzania (TWEA) Kanda ya Kaskazini kimeiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuwaachia wanachama wao waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwa tuhuma za kusafirisha tumbili hai 62 bila vibali huku wakieleza kuwa wapo tumbili wengine katika mabanda yao.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Arusha Bird Traders na raia wawili wa Uholanzi waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakituhumiwa kusafirisha tumbili hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana hapa, Mwenyekiti wa Twea Kanda ya Kaskazini, Othman Bhoki alisema kukamatwa kwa raia hao wawili KIA ambao ni Arten Vardanian (52) na Edward Vardanian (46) pamoja na Idd Misanya ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni iliyotumika kukamata tumbili hao ya Arusha Bird Traders ni kuwarudisha nyuma wafanyabiashara ambao wana vibali halali vya kuvuna tumbili hao.
Alisema wasafirishaji wa tumbili hao ambao ni Kampuni ya Arusha Bird Traders wana vibali halali vya kufanya biashara hiyo kwa maelekezo ya tangazo la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Alisema suala hilo ni vyema likachunguzwa kwa kina kwani kampuni hiyo imewasilisha kibali halali cha kusafirisha wanyama hao chenye namba 29655 (Cites) kilichotolewa Februari 24, mwaka huu ambacho kinamalizika muda wake Agosti 23, mwaka huu.
Alisema kibali hicho kimeruhusu tumbili 62 kusafirishwa kwenda nchini Armenia na kukamatwa kwao kunaleta mkanganyiko kwani kwa mujibu wa kibali cha kukamata wanyama hao, kinaonesha kuruhusu daraja namba 13 la kuruhusu gawiwo la tumbili kuuzwa nje ya nchi.
Alisema aina ya tumbili waliozuiwa wapo katika mgawo wa Taifa iliyoruhusu wauzwe tumbili 5,000 kwa mwaka na wafanyabiashara na gawiwo hilo kwa daraja tajwa lina tumbili aina mbili; Velvet Monkey na Blue Monkey (400).
Alisema katika mazingira hayo wanashindwa kuelewa ni vigezo gani alivyotumia Waziri wa Maliasiali na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kuzuia wanyama hao kwenda nje ya nchi kwani daraja lililokatazwa kufanyiwa biashara ni la 14 ambalo linahusu wanyama wakubwa hasa wale wenye pembe na kwato.
Alisema kinachoshangaza zaidi wakati tumbili hao wakizuiwa kusafirishwa huku wakurugenzi wakishikiliwa na Polisi, wanachama hao wa TWEA Kanda ya Kaskazini bado wana tumbili katika mabanda yao wanaosubiri kusafirishwa nje ya nchi katika masoko mbalimbali barani Ulaya.
“Tunalaani kuitwa watoroshaji wa wanyama hawa wakati tuna vibali vinavyoturuhusu kusafirisha wanyama hawa tunaomba uchunguzi wa kina juu ya suala hili ili tujue hatma ya raia hao wanaoshikiliwa na polisi maana hapa kuna mkanganyiko na hatujui Waziri Maghembe amezuia kwa kibali gani ni hiki tulichonacho au la,” alisema.
Naye Katibu wa Twea, Said Gumbo alisema kwa hatua hiyo ya Wizara kuzuia wanyama hao, wafanyabiashara hao wamewekwa katika mazingira magumu kwani wanaofanya biashara hiyo ni raia wa Tanzania wanaotafuta riziki zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.
Aliiomba Serikali kufanya uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na kuwaachia wanachama hao wanaoshikiliwa. Mwishoni mwa wiki, vyombo vya ulinzi na usalama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) viliwanasa wafanyabiashara wawili ndugu raia wa Uholanzi wakijaribu kusafirisha tumbili kwenda nchini Armenia.
Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa Belarus kupitia Kampuni ya Arusha Freight Limited ya hapa.
Mbali ya raia hao wa Uholanzi pia wanamshikilia Mtanzania, Misanya ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni iliyotumika kukamata tumbili hao ya Arusha Bird Traders anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na wamehifadhiwa Kituo cha Polisi KIA huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea.

Wanasayansi wadai povu la chura ni tiba

No comments

Wanasayansi wadai povu la chura ni tiba


Povu la churaGLASGOW, UINGEREZA
WANASAYANSI nchini Uingereza wamesema povu linalotolewa na vyura wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao linaweza kuponya majeraha ya wagonjwa walioungua kwa moto.
Pia wanaamini kuwa povu hilo linaweza kukusanywa na kusaidia mchakato wa matibabu kama kizuizi baina ya bandeji na ngozi iliyoungua.
Watafiti kutika Chuo Kikuu cha Strathclyde wameanza utafiti juu ya povu hilo linalotolewa na vyura wadogo kutoka kwenye kisiwa cha Tungara, huko Trinidad.
Vyura hao hutoa povu la urefu wa sentimita 5 kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano.
Povu hilo limetengenezwa kwa aina tano za protini.
Doctor Paul Hoskisson na wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini zinazopatikana kwenye povu hilo na kuchanganya na dawa zao ili kuipata tiba husika.
Watafiti hao watawasilisha kazi yao katika mkutano wa mwaka wa kituo cha uratibu wa shughuli za utafiti wa viumbe hai -Microbiology Society- utakaofanyika Liverpool.

Askofu amwangukia Magufuli

No comments

Askofu amwangukia Magufuli


Pg 1
>> Viongozi wa dini wasisitiza upendo, umoja katika familia
NA MWANDISHI WA GAZETI LA MTANZANIA, DAR ES SALAAM
ASKOFU wa Kanisa la Anglikani nchini (KAT), Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Askofu Stanley Hotay, amesema kanisa halina majipu ya kutumbuliwa kwa kuwa linatoa huduma zinazoisaidia Serikali kupeleka maendeleo kwa Watanzania.
Kauli ya Askofu Hotay aliyoitoa mjini hapa jana wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid imekuja wakati mwenendo wa uongozi wa Rais John Magufuli ni wa kutumbua majipu kutokana na kile alichokisema Februari, mwaka huu wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam kuwa alikuta uozo mkubwa serikalini.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi katika ibada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, Askofu Hotay alipongeza juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Magufuli.
Askofu Hotay ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Kanisa la Arusha alisema kumekuwapo na taarifa
za waraka wa kuondolewa kwa misamaha ya kodi kwa kanisa hatua aliyosema kama itatekelezwa itarudisha nyuma
juhudi za kuisaidia Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
“Tunakuomba mkuu wa mkoa utusaidie kufikisha hili. Lakini pia liangaliwe vizuri sisi hatuna majipu kabisa.
Tunasaidiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii,” alisema Askofu Hotay.
Kwa upande wake, Ntibenda, aliwaomba viongozi wa kanisa kuisaidia Serikali kuhamasisha vijana kufanya
kazi.
“Rais Magufuli amenipa majukumu ya kuhakikisha watu wanafanya kazi hasa vijana badala ya kucheza mchezo wa pool.
Tabia hii ikiachwa itatengeneza Taifa la wavivu na walalamikaji,” alisema Ntibenda.
Alisema Serikali itaendeleza ushirikiano uliopo baina yake na taasisi za dini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu
wake wanaendelea kuabudu kwa amani na utulivu.
Katika ibada hiyo, Ntibenda, alilazimika kutoa namba yake ya simu ambayo ni 0766030000 na 0754604003
baada ya kuwataka wananchi wasikubali kutoa rushwa katika maeneo ya huduma za kijamii.
“Nawaomba wananchi nipigieni simu pindi mnapoombwa rushwa katika huduma za kijamii na maeneo mengine.
Nisaidieni kupambana na vita hii,” alisema Ntibenda ambaye namba yake ilisomwa kwa wananchi na Askofu Hotay.
MAGUFULI
Kwa upande wake, Rais Magufuli, aliwashangaza waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililoko Oysterbay jijini Dar  es salaam baada ya kusimamisha msafara wake na kisha kusalimiana na walemavu.
Tukio hilo lilitokea jana katika lango la kutokea kanisani hapo ambako alikwenda kuhudhuria Ibada ya Ijumaa
Kuu.
Magufuli alifika kanisani hapo mapema na kusali pamoja na waumini wa kanisa hilo na ibada ilipoisha alipanda katika gari lake na kuondoka.
Wakati akiondoka alikuwa akiwapungia mkono waumini hao na alipofika langoni hapo ghafla msafara wake ulisimama na kisha kushuka ili kuwasalimia waumini hao jambo lililowafanya wengine kusogea
ili kujua kilichotokea.
Magufuli alishuka na kuwafuata walemavu waliokuwa wamekaa jirani na lango hilo la kutokea na kuzungumza
nao.
Ingawa mazungumzo hayo hayakusikika, kitendo cha kushuka na kuzungumza na walemavu hao kiliwafanya watu waliokuwapo jirani na eneo hilo kuvutiwa na alipomaliza alipanda tena katika gari yake na msafara huo kuondoka kuelekea Ikulu.
Awali, akizungumza katika mahubiri hayo, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Stephano Kaombwe, aliwasihi
Watanzania kuwa na moyo wa upendo.
Huku akinukuu katika Biblia Takatifu katika injili ya Yohana, Kaombwe alisema inashangaza kwamba Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo kwa ajili ya wanadamu lakini wenyewe bado
wanachukiana.
“Wanadamu hatukuumbwa tuteseke, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona Mungu aliwaweka Adam na
Hawa kwenye bustani ili waishi vizuri, wastarehe lakini walitenda uasi,” alisema Kaombwe.
LOWASSA
Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyeshiriki ibada hiyo katika Kanisa la Azania Front Kanisa aliwatakia
Watanzania washerehekee Sikukuu ya Pasaka kwa amani lakini alikataa kuzungumzia ya Zanzibar.
“Suala la uchaguzi wa Zanzibar siwezi kulizungumzia kwa sasa labda hapo baadaye lakini kufanyika kwa uchaguzi
huo ninamtukuza Mungu,” alisema Lowassa baada ya ibada hiyo kumalizika.
Awali akizungumza katika ibada hiyo, Mchugaji wa Usharika wa Azania Front, Charles Mzinga, alisema ni vyema wazazi watekeleze wajibu wao katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora.
“Watoto wetu tunapaswa kuwalea katika maadili yanayompendeza Mungu,” alisema mchungaji huyo.
Alisema kila mtu anapaswa kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kila analolifanya linamtukuza Mungu ikiwa kazini
au katika jamii.
Wakati huohuo, katika mahubiri yake aliyoyatoa Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padre Nicholas Masamba, aliwataka Wakristo kuwajibika kutekeleza majukumu yao katika familia zao
na si kuwachia walimu peke yao.
“Tafakari hii ya kifo cha Yesu kusema yametimia, inarudisha swali kwetu ikitutaka tujiulize kuwa ni mangapi tumeyatimiza na sisi kwenye ngazi mbalimbali ikiwamo kazini, malezi ya familia na kwenye nafasi mbalimbali kama Wakristo,” alisema Padri Masamba.
Katika ibaada hiyo iliyohudhuriwa na waumini wengi akiwamo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema Wakristo wengi wamekuwa wakishindwa kutimiza majukumu yao katika
nafasi mbalimbali.
Habari hii imeandikwa na Faraja Masinde, Ruth Mnkeni na Veronica Romwald (Dar es Salaam) na Eliya Mbonea (Arusha)

KUTOKA  GAZETI LA MTANZANIA

Kwa nini tumbili, mijusi ni ‘dili’ Ulaya

No comments


Mjusi aina ya Agama
Mjusi aina ya Agama 


Mjusi aina ya Agama




Dar/Moshi.Siri ya utoroshaji wa wanyama na wadudu hai kutoka Tanzania kwenda nje ya nchi imebainika. Wamekuwa wakitumika katika nchi mbalimbali kwenye utafiti, mapambo na kitoweo.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu, umebaini matumizi hayo na kuwa wanyama wanaotakiwa kwa wingi ni mijusi ya bluu, kenge na tumbili wanaopelekwa katika nchi za Ulaya kupitia viwanja viwili vya ndege hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Herman Keraryo alisema mbali na wanyama hao, wengine wanaopelekwa nje ni jamii ya nyani, wadudu na ndege.
Alisema hakuna nchi ambayo imejitambulisha kipeke kununua wanyama hao, bali imekuwa ni biashara kati ya mzawa na mnunuzi.
Alipoulizwa kuhusu uhalali wa biashara hiyo, Keraryo alisema mfanyabiashara lazima awe na leseni inayotambuliwa na Serikali; “... na siyo kila ndege anasafirishwa au nyani, kuna aina ya ndege wasioruhusiwa ila kwa kutozingatia sheria, baadhi ya watu wanaivunja.” Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Tanapa, Gerald Bigurube alisema wanyama kama kobe na kakakuona nao wamekuwa wakisafirishwa zaidi kwenda Vietinam na China kwa matumizi ya chakula na dawa.
Alisema matumizi mengine ya wanyama hao wanaopelekwa Marekani na Ulaya yamekuwa ni kwa ajili ya shughuli za mapambo.
“Wanyama hai na wadudu kwa kifupi wana soko pana sana duniani na matumizi yake ni kama hayo lakini inakuwa vigumu kujua moja kwa moja wanapelekwa nchi gani,” alisema.
Bigurube alisema wanyama wengine wamekuwa wakipelekwa kwenye maeneo ya mafunzo ili watu wengine duniani wajifunze historia yao. Imeelezwa kuwa mijusi ya bluu ambayo inapatikana Tanzania pekee ndiyo inayotafutwa zaidi na kila mmoja umekuwa ukiuzwa kwa Euro 5,000 (Sh12.2 milioni.)
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ndani ya Idara ya Wanyamapori, wimbi la ukamataji na utoroshaji wa mijusi hiyo na tumbili linatokana na kuhitajika katika nchi mbalimbali kwa ajili ya utafiti.
“Kitu kinachoibwa zaidi sasa hivi nchini ni hao tumbili kwa sababu wanatumika sana huko nje kwa ajili ya utafiti wa kitabibu,” kilidokeza chanzo chetu na kuongeza: “Hata unavyoona, faru wanauawa ni kwamba wenzetu huko nchi za Asia wanaamini unga wake unasaidia kuongeza nguvu za kiume.”
Matumizi hayo yamebainika siku chache baada ya vyombo vya dola kuwashikilia raia wawili wa Uholanzi kwa kosa la kusafirisha tumbili 61 ambao walikuwa wapelekwe Albania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).
Habari zilizopatikana juzi zilidai kwamba mmoja wa maofisa wanyamapori alipewa bakshishi ya Dola 3,000 za Marekani, sawa na Sh6.4 milioni za Tanzania katika ‘dili’ hiyo ya tumbili 61.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alikiri kuwa tumbili na mijusi hao wa bluu ndiyo wanaowindwa zaidi kwa sasa; “... na huyo Williams Blue Lizard ni mjusi anayepatikana Kimboza na Ruvu. Ndiyo maeneo pekee duniani. Huyo mjusi anakaa juu ya miti kwa hiyo wanachofanya ni kukata mti na kuuangusha ndipo wanawakamata na kuwaweka kwenye mabegi. Wanafanya uharibifu mkubwa.”
Profesa Maghembe alisema mijusi hao huuzwa kati ya Euro 5,000 hadi 6,000 kila mmoja katika nchi za Ulaya.
Kuhusu tumbili, Profesa Maghembe alisema mpango ulikuwa ni kukamata tumbili 441 kwa awamu lakini kikwazo kikubwa kilikuwa ni upatikanaji wa kibali cha kuwasafirisha kwenda nje.
Alipoulizwa kwa nini raia hao wa Uholanzi wamekamatwa wakati walikuwa na kibali, alisema kibali hicho kilitolewa katika mazingira ya rushwa.
“Ni kweli walikuwa na kibali lakini kilitolewaje wakati nilishazuia na waraka ukatolewa? Lakini ujue hawakuwa na kibali pia cha kuwakamata hao wanyama,” alisema.
“Hili jambo lina njama kubwa na ndiyo maana tumeamua lichunguzwe na kile kikosi kazi cha kitaifa ambacho huchunguza makosa makubwa ya kihalifu,” alisisitiza.


Kutoka katika gazeti la

Mwananchi

Thursday, March 24, 2016

Ozil akanusha kutaka kuondoka Arsenal

No comments

Ozil akanusha kutaka kuondoka Arsenal

OzilLONDON, ENGLAND
KIUNGO wa timu ya Arsenal, Mesut Ozil, amekanusha uvumi kwamba ataondoka katika kikosi hicho kama kocha Arsene Wenger ataendelea kuwepo.
Ozil amedai kwamba kwa sasa yupo katika klabu hiyo kutokana na uwepo wa kocha huyo na uhusiano wao kuwa mzuri.
Mtandao wa Don Balon wa nchini Hispania, ulitoa taarifa kwamba, mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Ujerumani amechoka kuitumikia Arsenal kutokana na kukosa mafanikio katika Ligi Kuu nchini England kwa muda mrefu na amepanga kurudi Hispania katika La Liga.
Habari hiyo imemfanya Ozil ajisikie vibaya, ila amedai kwamba hakuna ukweli wowote juu ya kauli hiyo na anamheshimu kocha wake, Wenger.
“Nashangaa kuona vyombo vya habari vikiandika mambo ambayo hayana ukweli, ninamheshimu Wenger na nipo Arsenal kwa ajili yake,” alisema Ozil.
Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo 2013, akitokea Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 42.5 hadi sasa mchezaji huyo amefanikiwa kutwaa taji la Kombe la FA tangu alipojiunga na timu hiyo.

Monday, March 14, 2016

UWEZO WA NGISI KUJIBADILI RANGI

No comments
                                    UWEZO WA NGISI KUJIBADILI RANGI

Ngisi anayeitwa cuttlefish ana uwezo wa kujibadili rangi na ujificha hivi kwamba asiweze  kuonwa na mwanadamu .Kulinga na ripoti moja ,Ngisi hao "wanafahamika kuwa na rangi mbali mbali na wanaweza kubadili rangi kwa njia ya kustahajabisha".

Ngisi huyo ujibadili rangi kwa kutumia chembe chembe fulani ndogo za pekee zilizo chini ya ngozi yake.Chembe hizo huwa na vifuko vilivyo jaa rangi mbalimbali vilivyo zungukwa na misuli midogo sana.
Ngisi uyo anapo taka kujibadili rangi ili ajifiche,Ubongo wake utumatahalifa ya kukaza misuli ilio zunguka vifuko ivyo,kisha vifuko ivyo na misuli utanuka na rangi ya ngisi ubadilika mara moja.Mbali na kutumia uwezo uwo kwa kujificha ,Pia utumia uwezo huo kuvutia ngisi wengine na ata kuwasiliana nao.
Wataalamu katika chuo kikuu cha Bristol Ungereza Walitengeneza ngozi  ama ya Ngisi huyo,Waliweka vsahan vya mpira mweusi katika vitundu vidogo vinavyo fanya kama misuli ya ngisi uyo ,Watafiti hao walipo unganisha umeme katika ngozi iyo,Misuli iyo ilitanuka na kubadili rangi ya ngozi iyo.
Utafiti ulio fanya kuusu ngozi ya Ngisi uyo unaweza kutumia kutengeneza nguo ambazo uweza kubadili rangi,
JONATHAN ROSSISTER alifafanua misuli iyo uwa " lain na iimebuniwa kwa ustadi wa hali ya juu",
Na kusema ipo siku moja watu watavaa nguo zilizo buniwa na kutengenezwa kwa kutegemea muundo wa ngozi ya Ngisi uyo "CUTTLEFISH" zinazo weza kubadili rangi ,iwe kwa kujificha au mtindo.
                                                     
                                                            video

                      Click hapa kuona video
               

Thursday, March 3, 2016

Sanches asema asernal hawajiamini

1 comment
          hii ni mara  baada  ya arsenal  kushindwa  kuchomoka  wakiwa  ndani  ya  uwanja  wao  wa  emirates  mbele  ya swansea  kwa  kukubali  kichapo  cha  goli  2-1 kutoka  kwa Wayne Routledge na Ashley Williams hii ni  pamoja  na  arsenal  kuwa  wa  kwanza  kupata  goli  kutoka  kwa  mchezaji  wao  Joel Campbell katika dakika ya 15  mchezo.
  hivyo  mchezaji huyo  wa  arsenal Alexis  sanchez  alisema  "nadhani  tunaweza kushinda kombe  hili  la ligi na  wachezaji  tulionao  lakini  kuna  aina  fulani  ya  njaa tunaikosa  tunapokua  uwanjani, tunatakiwa  kuingia  uwanjani  tukiwa  kama  watu  ambao  tumeshafungwa  goli  moja  mbele  ili tupate  ari na  kasi ya kutafuta  ushindi"
"naukumbuka  ssana  mchezo  kati yetu  na  manchester united mwaka jana  tuliingia  tukiwa  na  njaa ya  magoli  kitu  ambacho kilifanya  timu  kucheza  kwa  nguvu zote  na  kasi  ya  kushambulia  kiasi kwamba  ndani  ya  dakika  ishirini tu  tulikua  tumeshapata  magoli matatu mbele"aliongeza  alexis sanches,
hivyo  sanches alimaliza  kwa  kusema  kuwa  anadhani  waoo kama arsenal  wanakosa  kujiamini  kama  wanaweza  kuwa  mabingwa  wa  ligi  hiyo  kwa  msimu  huu wa 2015/1016.
kwasasa  ligi  kuuu uingerza  inaongozwa   na  leicister city  kwa  point 57 ambaye  pia alishindwa  kupata  ushindi akiwa  nyumbani   na  kuambulia suluhu ya 2-2 dhidi  ya  west brom, ikifuatiwa  na  Tottenham kwa  pointi 54 mara  baada  ya  kukubali  kichapo  cha  goli  1-0 kutoka  kwa  west ham.....

Friday, February 26, 2016

mlipuko kwenye sherehe za Uzinduzi wa kanisa katoriki parokia ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi

No comments
mlipuko kwenye sherehe za Uzinduzi wa kanisa katoriki parokia ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 60 wamejeruhiwa kati yao 42 hali zao ni mbaya baada ya kutokea mlipuko kwenye sherehe za Uzinduzi wa kanisa katoriki parokia ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi -Olasiti jijini Arusha.

                          

BASI LA MASHIMBA EXPRESS LAPATA AJALI MBAYA

No comments
Basi La Mashimba Express La Kutoka Kahama na kwenda Mwanza Lagongana Na Gari Ndogo Na Kuua Watu  Wanne


Watu wanne wamefariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo  katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu  Mkoani Shinyanga

Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ilisababishwa  na  gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu  wawili  waliokuwa  katika  gari  hilo  akiwemo  dereva  walifariki  dunia  papo hapo


Mganga mfawidhi wa hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo  walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.

Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi .

Thursday, February 25, 2016

PATA NENO

No comments

PATA NENO


 "Ucjisifu una marafik wengi kama nywele zako wkt wa shida utajikuta KIPARA". Na huu ndo ukwl wnyw na waliopitia na wanaoendelea kupitia hali hii watakubaliana nami.
By Matanza.....

Mwanamume Afumaniwa Akila Uroda Na Ng'ombe, Limuru

No comments

Mwanamume Afumaniwa Akila Uroda Na Ng'ombe, Limuru

Ni kitendo cha kushangaza.Mwanamume kufanya ngono na ng'ombe.Hili ndilo jambo lililoshuhudiwa hii leo katika kijiji kimoja huko Kiambaa baada ya jamaa anayefanya kazi na kampuni ya maji ya Kikuyu, kufumaniwa akifanya kitendo hicho kisicho cha kawaida na ngombe katika mojawapo ya boma la eneo hilo.

picture




Ng'ombe agoma kufa baada ya kuchinjwa

No comments

Ng'ombe agoma kufa baada ya kuchinjwa


picture



Wednesday, February 24, 2016

MTU AJIITA MUNGU ATOKEA UKO DRC KONGO

No comments
MTU AJIITA MUNGU ATOKEA UKO DRC KONGO 

Nitukio la kushangaza na kusisimua sana lililo tokea Uko JAMUULI YA DEMOKRASIA YA KONGO,
 mji wa Gavilan  katika kanisa la Tatu la malkia wa ubembe.
(Picture yake)
(NabiiaTATA WAHISEELELWA)

, Mtu moja Afahamikae kwa
jina la Nabiia WATATA WAHISEELELWA Ajiitae MUNGU 3 yani Mungu Mtu Roho Mtakatifu,
Mtu uyo(Nabiia WATATA WAHISEELELWA) amedai Amekuja kama Musa na Yesu walivyo kuja,
Nabiia WATATA WAHISEELELWA asema Yesu na Musa walikua wazungu ila yeye ni mweusi 
Adai uwo ndio utatu mtakatifu

(Video)

Monday, February 22, 2016

Mtoto azaliwa na vichwa vitatu..

No comments

   Mtoto azaliwa na vichwa vitatu

               Mtoto mwenye vichwa vitatu azaliwa katika hospital ya 
GARISSA,yasemekana mtoto uyo amezaliwa na vichwa vitatu
 ,vidole sita na akiwa na meno..
 (video)


                                                                   

Angalia mazingaombwe ya wazungu

No comments
Angalia mazingaombwe ya wazungu


ajali mbaya iliyotokea bara la Asia

No comments

ajali mbaya iliyotokea bara la Asia

                                                                                                            

MATUKIO UK WACHAWI WANASWA KATIKA KANISA LA UFUNUO JIJINI MWANZA

No comments

MATUKIO UK WACHAWI WANASWA KATIKA KANISA LA UFUNUO JIJINI MWANZA

Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 asubuhi leo katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.


KILICHO MKUTA SHABIKI WA YANGA

No comments
KILICHO MKUTA SHABIKI WA YANGA 
Hii ni baada ya February 20/2016 ilichezwa mechi ya Yanga vs Simba uwanja wa taifa Dar es salaam ,Ni mechi ya ligi kuu ambapo Yanga walichukua ushindi wa 2-0, ikiwa ni mara ya 31 Yanga kuishinda Simba ikiwa hii ni mechi yao ya 81 toka waanze kukutana uwanjani.

Baada ya mpila kuisha washabiki video


Friday, February 19, 2016

Samaki Watembeo inch kavu

No comments
Samaki Wanao tembea inch kavu
SSamaki Wanao tembea inch kavu 
Kiukweli Dunia inaviumbe wengi na waajabu sana;

(video)

                             
No comments
 CHEZEA UJANA

Binti mmoja wa kitanzania alikuwa anasomea masomo ya kisayansi huko china muda wa miaka 20 alipofuzu na akaweza kugundua dawa ya kutozeeka akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa wanywe tone moja moja wasizeeke,baada ya miaka 20 aliporudi tanzania alimkuta mama yake kawa binti huku kabeba kitoto cha kiume kidogo mgongoni akafurah kumkuta mama yake kawa binti akamuulza baba yuko wapi?
Mama akajibu mwanangu baba yako alivyoniona nimekunywa dawa nimekuwa binti yeye akanywa kichupa chote ndo huyu nimembeba mgongoni!

binti akazimia pale pale!
by francnho

Thursday, February 18, 2016

WAZO LA LEO

No comments
 WAZO LA LEO: 


WAZO LA LEO:
Hata uwe na tamaa vipi huwezi kutamani kifo.......!!
WAZO LA KESHO; mwanaume hata awe na huruma vipi, hawezi kumsaidia mwanamke kubeba mimba.
WAZO LA KESHO KUTWA; Urefu na ufupi ni majaliwa ya muumba lakini vitambi na mimba ni juhudi zetu wenyewe! 

UKWELI WA MAISHA.
Bila pesa Mademu wazuri Utaishia Kuwaita Shemeji.......!

NI MTAZAMO TU,, 



Mapenzi yangekuwa IBADA vijana wote 2ngeenda MBINGUNI.

BINADAM NI JINO

No comments
 BINADAM NI JINO

Hivi Kila Binadam Ni JINO? Maana MTU akifa Wanasema Kaacha Pengo..

by francnho

DEREVA MPENDA NGONO..

No comments
 DEREVA MPENDA NGONO

DEREVA mpenda Ngono alimpa lifti SISTER wa Kanisa. kila akibadili Gia Mkono wake unagusa Paja la Sister. Yule Sister akamwambia soma "Mathayo 7:7 DEREVA kusikia hivyo akamuacha kumgusa huku akijiuliza Mathayo 7 inasemaje?. Alipomfikisha Kanisani, Jamaa karud nyumban akachukua Biblia na kupekua Mathayo 7:7 na kukutana na Ujumbe usemao "OMBENI NANYI MTAPEWA" Jamaa daaah nimekosa JE dereva alikosa nin! tujifuze kuomba.

by francnho

CHEZEA UJANA..

No comments
 CHEZEA UJANA


Binti mmoja wa kitanzania alikuwa anasomea masomo ya kisayansi huko china muda wa miaka 20 alipofuzu na akaweza kugundua dawa ya kutozeeka akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa wanywe tone moja moja wasizeeke,baada ya miaka 20 aliporudi tanzania alimkuta mama yake kawa binti huku kabeba kitoto cha kiume kidogo mgongoni akafurah kumkuta mama yake kawa binti akamuulza baba yuko wapi?
Mama akajibu mwanangu baba yako alivyoniona nimekunywa dawa nimekuwa binti yeye akanywa kichupa chote ndo huyu nimembeba mgongoni!


binti akazimia pale pale!
by francnho

CHEZEA UJANA

No comments
 CHEZEA UJANA


Binti mmoja wa kitanzania alikuwa anasomea masomo ya kisayansi huko china muda wa miaka 20 alipofuzu na akaweza kugundua dawa ya kutozeeka akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa wanywe tone moja moja wasizeeke,baada ya miaka 20 aliporudi tanzania alimkuta mama yake kawa binti huku kabeba kitoto cha kiume kidogo mgongoni akafurah kumkuta mama yake kawa binti akamuulza baba yuko wapi?
Mama akajibu mwanangu baba yako alivyoniona nimekunywa dawa nimekuwa binti yeye akanywa kichupa chote ndo huyu nimembeba mgongoni!


binti akazimia pale pale!
by francnho

CHEZEA UJANA

No comments
 CHEZEA UJANA


Binti mmoja wa kitanzania alikuwa anasomea masomo ya kisayansi huko china muda wa miaka 20 alipofuzu na akaweza kugundua dawa ya kutozeeka akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa wanywe tone moja moja wasizeeke,baada ya miaka 20 aliporudi tanzania alimkuta mama yake kawa binti huku kabeba kitoto cha kiume kidogo mgongoni akafurah kumkuta mama yake kawa binti akamuulza baba yuko wapi?
Mama akajibu mwanangu baba yako alivyoniona nimekunywa dawa nimekuwa binti yeye akanywa kichupa chote ndo huyu nimembeba mgongoni!


binti akazimia pale pale!
by francnho

hot weekly news

toniking wed designer

toniking wed designer